Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584566

Soccer News of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

PSG, Lyon hakuna mbabe

PSG, Lyon hakuna mbabe PSG, Lyon hakuna mbabe

Vinara wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1 Paris St-Germain wameambulia alama moja kufuatia sare ya goli 1-1 na Lyon katika mchezo wa Ligi uliopigwa Jumapili.

Wenyeji wa mchezo huo Lyon walianza vyema na kupata bao kupitia kwa Lucas Paqueta kabla ya bao hilo kusawazishwa ungwe ya pili kunako dakika za jioni kupitia kwa Thilo Kehrer.

Ushindi huo unaifanya PSG kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligue 1 kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya timu iliyo nafasi ya pili Nice wakati Lyon wanashika nafasi ya 11 ikiwa ni sare ya nne mfululizo.