Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560245

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

PSG yaichapa Man City, Messi akifunga bao lake la kwanza

Messi afunga goli lake la kwanza akiwa na PSG Messi afunga goli lake la kwanza akiwa na PSG

Baada ya msimu uliopita kupigwa nje ndani na kushindwa kufika fainali na Man City , PSG wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Parc De Princes wameiadhibu City magoli 2-0.

katika mchezo huo kama ilivyo ada kwa Lionel Messi anapokutana na Vilabu vya Uingereza na hasa Arsenal na Man City ametupia bao moja 74' na kufungua akaunti yake ya magoli ndani ya kikosi hicho.

Goli jingine la PSG limefungwa na Kiungo Gueye 8',na kuwahakikishia PSG kuondoka na pointi 3.

kwa matokeo hayo,PSG amefikisha Pointi 4 akiongoza Kundi A, sawa sawa na Clubb brugge.