Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 15Article 551593

Soccer News of Sunday, 15 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

PSG yapiga 4, Messi bado

Wachezaji wa Kikosi cha PSG Wachezaji wa Kikosi cha PSG

Katika muendelezo wa Ligue 1,Matajiri wa Jiji la Paris,PSG wameendelea kuonesha kiwango cha hali ya juu na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 katika dimba la Parc des Princes dhidi ya strasbourg.

Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko ,PSG walikua tayari washaingia nyavuni mara tatu mabao yakifungwa na Mauro Icardi,Mbappe na Julian Draxler.

Kipindi cha Pili Strasbourg walirudi kwa kasi na walipata magoli mawili ya haraka haraka yaliyofungwa na Kevin Gameiro na Ludovic Ajorque kabla ya Beki wao Alexander Djiku kupata kadi nyekundu na kuwadhoofisha.

Katika mchezo huo macho ya wengi yalikua yakisubiri kwa hamu kuona nyota wapya wa klabu hiyo wakianza kuitumikia jezi ya PSG, beki Sergio Ramos na "Mchawi mweupe" Lionel Messi lakini Mwalimu Mauricio Pochettino hakuwajumuisha kabisa kwenye kikosi.