Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 585967

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Pablo: Tumetimiza Malengo Mapinduzi Cup

Pablo: Tumetimiza Malengo Mapinduzi Cup Pablo: Tumetimiza Malengo Mapinduzi Cup

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amefunguka kuwa lengo alilopanga kulipata kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi limetimia kwa asilimia 100 na sasa akili yake inahamia kwenye mipango mingine.

Pablo alisema licha ya kuwa walikuwa wanahitaji kupata ubingwa wa Mapinduzi, kitu kingine alihitaji kuwaona wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye ligi kuu, huku akihitaji pia kuwajaribu wachezaji wa kigeni ambao walikuja kwa ajili ya majaribio.

Pablo alisema kuwa wachezaji wote ambao alikwenda nao kwenye michuano ya Mapinduzi amewapa nafasi ya kucheza isipokuwa wagonjwa na sasa amejua wapi kwenye kikosi chake pana nguvu kubwa na sehemu gani kuna upungufu na hiyo itamsaidia kwenye kujenga timu yake.

“Malengo yaliyotuleta kwenye mashindano haya yametimia kwa asilimia 100, kwa sababu tulipanga kucheza fainali na tumecheza, tulihitaji kuwaona wachezaji wapya na imekuwa hivyo. Kilichobaki kwa sasa ni kutazama mipango mingine ambayo itakuwa na manufaa kwenye timu yetu,” alisema Pablo.

Pablo aliiongoza Simba kucheza fainali ya Kombe la Mapinduzi juzi usiku dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Amaan uliopo Zanzibar, ikiwa ni mara ya kwanza kwake kufanya hivyo mara baada ya kukaa kwa muda mfupi tangu alipopewa jukumu la kuinoa Simba.