Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584677

Soccer News of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Pablo aahidi burudani kwa Wanasimba leo, lakini atoa tahadhari

Pablo Franco Martin Pablo Franco Martin

Michuano ya Mapinduzi Cup kule Visiwani Zanzibar imefikia mahala patamu. Hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Michezo yote ya Nusu Fainali inapigwa leo Januari 10, ambapo Yanga watashuka dimbani majira ya saa Kumi jioni kukabiliana na Azam FC, wakati Simba SC wao watakua na kibarua kigumu mbele ya Namungo majira ya saa 2:15 usiku.

Sasa Kocha wa Wekundu wa msimbazi anajua kibarua atakachokwenda kukutana nacho mbele ya Namungo na alikuwa na machache ya kusema kuelekea katika mchezo huo.

"Kwetu itakuwa mechi ngumu lakini tutajaribu kucheza mchezo wetu bora sababu tumekuja hapa kuwapa furaha mashabiki wetu" amesema Pablo