Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572890

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: mwanaspoti

Pablo baada ya ushindi wa Ruvu afunguka "tunataka kushinda zote"

Pablo baada ya ushindi wa Ruvu afunguka Pablo baada ya ushindi wa Ruvu afunguka

Mchezo huo ambao ni wa kwanza kwa kocha huyo amesema ameridhishwa na matokeo hayo ambayo yatawapa vijana ujasiri wa kupambana katika michezo miwili ijayo dhidi ya Geita Gold, Yanga na michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba imeinyuka Ruvu Shooting kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa CCM Kirumba yakifungwa na Meddie Kagere (2), Kibu Denis na Elias Maguli akiifungia Ruvu bao la kufutia machozi.

Licha ya ushindi huo Pablo amesema hakufurahishwa na namna vijana wake walivyocheza kipindi cha pili wakishindwa kupachika bao lolote na kuruhusu bao moja.

"Bila kujali idadi ya mabao huu ushindi ni muhimu kwetu kwa sababu utarejesha hali ya kujiamini kwa vijana bado tuna mechi ziko mbele yetu na zote tunahitaji kushinda," amesema Pablo.

"Tuna michezo kama mitatu iko mbele yetu tunahitaji kufanyia kazi mapungufu lakini kiujumla nafurahishwa na wachezaji wangu wanavyowajibika uwanjani na kufanyia kazi yale tunayoyapanga japo bado safari ni ndefu lakini timu hii ina wachezaji wazuri," amesema.

Related Pablo apangua kikosi amrejesha Wawa, ampa kazi Kagere Pablo atuma salamu.. aanza na dozi ya tatu huko Barbara: Subirini muone Simba yatakata Kirumba, Kagere akiweka 2Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha alama 14 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 14 na mchezo mmoja mkononi utakaochezwa kesho dhidi ya Namungo.