Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573094

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Pawassa aahidi ubingwa COSAFA

Kocha wa Timu ya Taifa, Soka la ufukweni Boniface Pawassa Kocha wa Timu ya Taifa, Soka la ufukweni Boniface Pawassa

Timu ya taifa ya mchezo wa soka la ufukweni leo itacheza fainali ya mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini katika ufukwe wa South Beach Arena dhidi ya Msumbiji.

Tanzania imefuzu fainali baada ya kuifunga Angola kwa mabao 5-2 na Msumbiji iliifunga Afrika Kusini kwa mabao 5-3. Tanzania inakutana na Msumbiji kwa mara ya pili baada ya kukutana kwenye hatua ya makundi na kufungwa kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4 na Angola watacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na Afrika Kusini, ambapo wanakutana mara ya pili.

Walipokutana kwenye makundi Afrika Kusini walifungwa 4-1. Akizungumzia wa timu ya Tanzania, Boniface Pawassa alisema walikwenda kwenye mashindano hayo wakiamini watafanya vizuri lakini Msumbiji ni nzuri kwani imecheza fainali za Kombe la Dunia msimu uliopita.

“Tumejiandaa kwa mchezo wa fainali na tulikuja kwenye mashindano kwa ajili ya kuonesha ushindani, nashukuru Mungu tunacheza fainali. Nitakuja na mbinu tofauti katika mchezo huu kwa sababu Msumbiji ni wazuri kwa kila kitu lakini hata sisi ni wazuri ndio maana tumefika fainali,” amesema Pawassa.

Comoro inashika nafasi ya tano baada ya kuifunga Shelisheli kwa mabao 8-6. Mashindano hayo ambayo yalianza Novemba 17 yatafika tamati leo yakishirikisha timu kutoka katika mataifa ya sita ambayo yalipangwa katika makundi mawili. Kundi A lina Angola, Afrika Kusini na Shelisheli, Kundi B ni Tanzania, Msumbiji na Comoro.