Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 06Article 545647

Habari za michezo of Tuesday, 6 July 2021

Chanzo: dar24.com

Penati za Morrison zamkera MO

Penati za Morrison zamkera MO Penati za Morrison zamkera MO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ ameonyesha kukerwa na matukio ya Simba SC kunyimwa mikwaju miwili ya penati ya dhahiri katika mchezo dhidi ya Young Africans uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi Jumamosi (Julai 03).

Katika mchezo huo ambao Young Africans walipata ushindi wa bao 1-0, winga Bernard Morrison alihusika kwenye matukio mawili ambayo kwa hakika mwamuzi Emmanuel Mwandembwa melalamikiwa alipaswa kutoa adhabu ya penati.

Tukio la kwanza lililotokea kwenye kipindi cha kwanza baada ya krosi ya Morrison kumgonga mkononi beki Dickson Job akiwa ndani ya eneo la hatari.

Lakini pia kwenye kipindi cha pili, Morrison alivutwa jezi na Deus Kaseke na kuangushwa ndani ya eneo la hatari lakini mwamuzi akapeta.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Mo amekumbushia matukio hayo huku akiwapa pongezi Young Africans kwa kupata alama tatu.