Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572473

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Presha imemwondoa Nchimbi Yanga

Ditram Nchimbi Ditram Nchimbi

Mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi amefunguka sababu za kushindwa kuwa mcharo ndani ya Yanga, ni presha ya mashabiki na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Nchimbi alijiunga Yanga msimu wa 2019/20 na ndani ya msimu huo ameifungia timu yake mabao mawili na asisti tatu, huku msimu uliofuata alifunga bao moja na asisti tatu na msimu huu hajagunga wala kutoa asisti.

Mkataba wa Nchimbi unamalizika Desemba 15 mwaka huu na tayari ameaga klabuni hapo na kwa sasa yupo likizo na muda ukifika ataweka wazi hatma yake kwenye soka.

Nchimbi alisema yupo kwao Tunduru na anafurahia maisha. Kuhusu soka bado ana muda wa kuendelea kucheza na kuthibitisha hilo amesema ana ofa zaidi ya tano mkononi.

“Siwezi kutaja ni timu gani hadi sasa zimenifuata, ila baada ya dirisha dogo nitaonekana uwanjani na natarajia kuwa bora zaidi kwani nitapata timu ambayo nitakuwa na uhakika wa kucheza mara kwa mara,” alisema na kuongeza;

“Kushindwa kufanya vizuri Yanga haina maana kiwango changu kimeisha, sio kweli nilienda timu yenye presha na kukosa muda wa kucheza mara kwa mara. Nina imani nikipata timu itakayonipa nafasi ya kucheza nitarudi kwenye ushindani,” alisema.