Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585826

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

RS Berkane yakata mzizi wa fitina kuondoka kwa Chama

Chama aamua kurudi nyumbani, Simba SC Chama aamua kurudi nyumbani, Simba SC

Klabu ya Berkane ya nchini Morocco imethibitisha kuondoka kwa mchezaji Clatous Chama ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo.

Berkane imesema Chama raia wa Zambia aliomba kuondoka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo familia, kushindwa kuendana na hali na maisha ya Morocco.

Chama ametambulishwa leo na klabu ya  Simba ambayo aliitumikia kwa mafanikio makubwa ikiwemom kubeba mataji ya Ligi Kuu.

Berkane inayonolewa na kocha Florent Ibenge  imemtakia heri na mafanikio Chama katika klabu yake ya Simba ambayo alitokea kwenda Morocco