Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552730

Tennis News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Rafael Nadal nae nje mwaka mzima, kuikosa US Open

Rafael Nadal nae nje mwaka mzima, kuikosa US Open Rafael Nadal nae nje mwaka mzima, kuikosa US Open

Bingwa mara nyingi wa michuano ya grandslam, Rafael Nadal raia wa Hispania amethibitisha kuwa atakosekana kwenye michuano ya Tenisi ya US Open inayotaraji kufanyika Agosti 30 mwaka huu nchini Marekani kwasababu anahitaji muda wa mwingi wa kupumzika baada ya kusumbuliwa na maumivu ya mguu.

Nadal ambaye pia ni bingwa mara tano wa michuano hiyo, amesema uamuzi wa kujitoa kwenye michuano hiyo umekuja baada ya kufuata ushauri kutoka kwa familia yake na jopo la matabibu ambao wamemfanyia vipimo na kugundua nyota huyo anahitiaji muda wa mwaka mzima kujiuguza

Nadal mwenye miaka 35, anaungana na bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Dominic Thiem kutoka Australia ambaye jioni ya jana alithibitisha kuwa hatoshiriki kwenye mashindano hayo baada ya kujitonesha kwenye mkono wake hivyo atakuwa nje pia kwa mwaka mzima.