Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573097

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Raga warudi kwa kasi

Mchezo wa Raga kurejea nchini Mchezo wa Raga kurejea nchini

Chama cha mchezo wa Raga (TGU) Tanzania kimedhamiria kufufua mchezo huo baada ya serikali kutaka kuona usajili wa klabu za mchezo huo nchi nzima.

Tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 2001 timu nyingi zilikuwa zinacheza mashindano kwa kujifurahisha kutokana na kusuasua kwake lakini awamu hii wameamua kufufua mchezo huo baada ya kupata klabu wanachama kutoka mikoa tofauti nchini.

Akizungumza kwenye mashindano ya klabu yaliyofanyika Uwanja wa TPDC, Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama hicho Jacob Jonas alisema wamerudi kwa kufanya mashindano ya klabu yaliyoshirikisha timu saba ili kuutangaza mchezo huo. “Kuna mpango tulianzisha wa kusajili klabu na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) walitaka kuona mashindano ndio maana tumeita timu zishindane kutoka Zanzibar, Mwanza, Dodoma, Arusha, Tanga, Dar es Salaam na Kilimanjaro,” alisema.

Jonas alisema anatarajia ndani ya miaka mitano ijayo watakuwa na timu imara ya taifa itakayoenda kushindana katika michuano ya kimataifa. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa chama hicho Eric Mulamula ambaye amewahi kucheza mchezo huo katika ligi ya Uganda alisema wanataka kukuza mchezo huo na kuuinua.

Alisema mchezo huo umekuwa na changamoto hasa viwanja na hivyo, kuhimiza wadau mbalimbali ambao wako tayari kutengeneza miundombinu wafanye hivyo kuwasaidia kushiriki kikamilifu. Miongoni mwa washiriki katika mashindano hayo ni Nyabitwano Thomas kutoka klabu ya Paja Pirates Zanzibar alisema kukufuliwa kwa mchezo huo kutasaidia kupatikana vipaji vingi vipya.

Katika mashindano hayo ya siku moja baadhi ya timu zilizocheza mapema Dar es Salaam ilipata ushindi wa mabao 36-0 dhidi ya Dodoma Dragons na Arusha Dumas walishinda mabao 38 -0 dhidi ya Tanga Titas.