Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572560

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Raiola: Disemba ni mwezi wa ndoto

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba

Mino Raiola wakala kiungo wa Manchester United Paul Pogba, amesema kwamba mchezaji wake atakuwa kwenye harakati za kuihama klabu ya Premier League kwenye dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatarajia kumaliza mkataba wake huko Old Traford mwezi Juni mwaka 2022 hivyo anaweza kuanza mazungumzo ya awali vilabu vingine kama hatoondoka Januari.

“Ni mapema sana kuongea kuhusu mkataba wa Pogba na Manchester United kwa sasa, acha tususbiri tuone nini kitatokea siwezi kumzuia yoyote kuota ndoto kuhusu yeye.” Raiola aiimbia TMW.

“Disemba ni mwezi wa ndoto na siwezi kuzuia lakini ni vyema kutoongea kuhusu Pogba, kama wachezaji wa zamani wa United hawaongei kuhusu mimi na Pogba hawawezi kufanya kazi tena.