Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585319

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rais Mwinyi Uwanjani kushuhudia Fainali Mapinduzi Cup

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye fainali za Kombe la Mapinduzi itakayozikutanisha Azam na Simba kesho kuanzia saa 2.15 usiku kwenye Uwanja wa Amaan.

Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano hayo Imane Osmond Duwe amesema kuwa kutokana na ukubwa na umuhimu wa mashindano hayo Rais ndiye atakayeyafunga.

Amesema kuwa utaratibu mzima kesho utabadilika ambapo Rais huyo atakuja na wageni wake kushuhudia fainali hiyo ambayo inazikutanisha timu hizo ikiwa zinakutana kwa mara ya tatu huku mara mbili Simba ikifungwa na  Azam FC.

Moja ya mabadiliko hayo ni katika uuzwaji wa tiketi za mechi ambapo sasa kutakuwa na tiketi 50 pekee za VVIP huku zingine zitabaki kuwa Sh 3000, 5000 na 10000.

"Hao 50 ndiyo watakaoingia kupitia pale VIP lakini wengine wote watapewa utaratibu maalumu wa kuingia ila tunawaomba mashabiki wafike mapema kuepuka msongamano.

"Rais wetu Hussein Mwinyi ndiye atatufungia mashindano hayo ambapo atakuwa na wageni wake wa kiserikali wakiwemo makamu wake. Viingilio vilivyobadilika ni tiketi za VVIP ambazo ni maalumu kwa baadhi ya watu," amesema Imane