Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 15Article 542857

Habari za michezo of Tuesday, 15 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Rais Samia ajibu ombi la Mbunge wa Makete

Rais Samia ajibu ombi la Mbunge wa Makete Rais Samia ajibu ombi la Mbunge wa Makete

Wiki chache zilizopita Mbunge wa Makete Festo Sanga alisimama Bungeni kumuomba Rais aingilie kati swala la Viwanja vya mpira wa miguu nchini vinavyomilikiwa na CCM ambavyo vimegubikwa na changamoto katika uboreshwaji wake lakini pia aliomba Rais afute kodi katika nyasi bandia ili kuboresha viwanja.

“Tunaomba Rais atusaidie viwanja hivi viwekwe nyasi bandia ilivisaiidie kukua kwa michezo nchini”>>> Sanga

Leo Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Vijana wa Tanzania jijini Mwanza, amejibu kilio cha Sanga na wanamichezo nchini kwa Kuagiza Wamiliki wa Viwanja (CCM) kuanza mchakato mara moja wa kuweka nyasi bandia kutokana na fursa ya kufutwa kwa kodi ya nyasi hizo na kama wameshinda wawape wawekezaji binafsi.