Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 08Article 561964

Soccer News of Friday, 8 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rashford atunukiwa Shahada ya Udaktari

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford

Nyota wa England na Manchester United Marcus Rashford ametunukiwa Shahada ya juu ya heshima kutoka chuo cha Manchester katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Old Trafford.

Rashford mwenye umri wa miaka 23, ni mwanaharakati anayepinga Ubaguzi,Umasikini na njaa kwa watoto.

Rashford ametunikiwa Udaktari wa heshima na chuo kikuu cha Manchester kwa harakati zake zinazoigusa jamii.

Baada ya kutunukiwa Shahada hiyo, Rashford ameweka rekodi ya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kutunukiwa.

Harakati za Rashford zinakubalika na wengi na miezi michache iliyopita alizungumza na rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.

Je jezi yake iandikwe Dr.Rashford? Ngoja tusubiri wiki ya EPL irudi