Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585178

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rasmi, Coutinho aungana na Gerrard Aston Villa

Phillipe Coutinho akitambulishwa ndani ya Aston Villa Phillipe Coutinho akitambulishwa ndani ya Aston Villa

Aston Villa wanajambo lao msimu huu. Toka kuuzwa kwa Jack Grealish, sajili zinazofanyika Villa Park ni moto! Philippe Coutinho amesajiliwa rasmi!

Coutinho amekamilisha usajili na sasa ni mchezaji rasmi wa Aston Villa akitokea FC Barcelona kwa mkataba wa mkopo (miezi 6).

Philippe anarejea Uingereza tangu alipoondoka Liverpool kwa gharama ya Euro milioni 146 Januari, 2018. Baada ya miaka 4, anarejea tena kwenye EPL akiwa chini ya Steven Gerard ambaye, waliwahi kucheza pamoja kule Anfield.

Villa wamelamba dume kwenye usajili huu. Uwepo wa Gerard pale Villa Park ni miongoni mwa kitu kilichomvuta Coutinho. Aston Villa watamlipa 50% pungufu ya mshahara aliokua analipwa Barca. Vilevile, wanauwezo wa kumsajili moja kwa moja kwa dau la Euro milioni 33 mwishoni mwa msimu huu.

Mchezo wa kwanza kwa Philippe ndani ya jezi ya Aston Villa unaweza kuwa ni dhidi ya Manchester United wikiendi hii pale Villa Park.