Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560167

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ratiba, mechi za UEFA Champions League

Mechi za UEFA, Septemba 28 Mechi za UEFA, Septemba 28

Ni vita ya kusaka pointi 3 muhimu kwa kila timu katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kusonga hatua ya 16 bora.

Usiku wa leo Septemba 28 kutakuwa na mechi nane za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya huku pia vigogo kadhaa wakishuka dimbani.

Real Madrid watakuwa nyumbani katika mchezo wa kundi D kuwakaribisha klabu ya FC Sheriff, huku Shakhtar wakiwakaribisha Inter Milan kutoka Italia.

Katika michezo ya kundi B, liverpool watakua ugenini kule Ureno kupepetana na Porto huku AC Milan wakiwakaribisha Atletico De Madrid.

Mchezo unsosubiriwa kwa hamu ni ule wa PSG dhidi ya Manchester City ambao utapigwa majira ya saa nne za usiku katika Uwanja wa Parc De Princes.