Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572806

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Real, Juventus wapigana vikumbo kwa Julian Alvarez

Julian Alvarez Julian Alvarez

Nyota wa River Plate Julian Alvarez emeingia kwenye rada za vilabu vya Juventus na Real Madrid.

Nyota huyu amekuwa kinara kwenye klabu ya River Plate kwa sasa, na kwa mujibu wa ripoti ya Marca nyota huyu amevivutia vilabu vyote viwili.

Wakala wa Alvarez, Fernando Hidalgo, anaripotiwa kuwa alikutana na klabu yake ya sasa kwa ajili ya mipango ya mkataba mpya.

Kwa mujibu wa ripoti, katika mazungumzo ya Hidalgo na klabu, imekubaliwa ada ya Euro milioni 20 kwa malipo ya mara moja kwa msimu ujao wa uhamisho ikiwa ni masharti ya staa huyu kuhamia Ulaya.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa staa huyu yeye hana haraka ya kutaka kuondoka. Na imani yake ni kuwa uwepo wake Argentina unamuweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kushiriki Kombe la Dunia.

Vilabu vya Fiorentina, Milan na Bayer Leverkusen pia vinaripotiwa kufuatilia kwa ukaribu maendeleo yake.

Wakati wake wa soka la kulipwa wote, Alvarez ameutumia kuwa na River Plate, akiwa amecheza mechi tano tu za timu ya taifa katika umri wa miaka 21.

Pia, Alvarez amechangia magoli 31 na asisti 23 kwenye mechi 90 akiwa na River.