Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558847

Habari za michezo of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Redondo Amewaka Kweli Kweli

Redondo Amewaka Kweli Kweli Redondo Amewaka Kweli Kweli

KIUNGO wa Biashara United Ramadhan Chombo (Redondo), Jumamosi iliyopita alionyesha kiwango cha juu baada ya kufunga mabao mawili wakati timu yake ya Biashara ilipowachapa FC Dikhil ya Djibout mabao 2-0.

Mbali na kufunga mabao hayo, kiungo huyo wa zamani wa Simba ameingia kwenye kitabu cha kuwa mchezaji wa kwanza wa Biashara United kufunga mabao mawili na kukosa penalti kwenye mchezo mmoja wa kimataifa.

Rekodi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba alionyesha kiwango hicho kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi FC Dikhil ya Djibout na kwenda hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-0. Kwenye mechi hiyo Redondo alikosa pia na penalti.