Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572650

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: eatv.tv

Rekodi zinaibeba Simba mbele ya Ruvu shooting

Simba waliifunga 3-0 Ruvu Shooting mara ya mwisho kucheza CCM Kirumba Simba waliifunga 3-0 Ruvu Shooting mara ya mwisho kucheza CCM Kirumba

Ligi Kuu soka Tanzania bara raundi ya 6 inaanza kutimua vumbi leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika mikoa tofauti, Ligi kuu inarejea baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili yakupisha kalenda ya kimataifa ya FIFA. Michezo yote ya leo inachezwa Saa 10 jioni.

Jijini Mwanza katika dimba la CCM Kirumba Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Simba SC. Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika uwanja huo ilikuwa Juni 3, 2021. Na mchezo huo ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0, mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco alifunga mara mbili na bao moja alifunga Chris Mugalu.

Huu pia utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha wa Simba Pablo Franco Martin kukiongoza kikosi hicho tangu atangazwe kuwa kocha wa timu hiyo, na kwa upande wa Ruvu shooting hawatakuwa na kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa ambaye amefungiwa michezo mitatu. Simba ipo nafasi ya 2 ikiwa na alama 11 wakati Ruvu shooting wana alama 6 wapo nafasi ya 10.

Katika Dimba la Ushirika Moshi mkoani Kilimamjaro Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Coastal Union ya Tanga. Costal ni miongoni mwa timu tano ambazo hazijashinda mchezo hata mmoja kwenye Ligi msimu huu wakiwa na alama 4 baada ya kutoka sare michezo 4 na kufungwa mchezo mmoja wakati wenyeji wao Polisi wana alama 10 kwenye michezo mitano wakiwa nafasi ya 3.

Na huko mkoani Rukwa katika Uwanja wa Nelson Mandela Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Mbeya Kwanza tofauti ya timu hizi kwanye msimamo ni alama 5 Mbeya kwanza wana alama 7 wakiwa nafasi ya 6 wakati Tanzania Prisons wanaalama 2 tu na hawajashinda mchezo hata mmoja wapo nafasi ya 15.