Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 14Article 551500

Habari za michezo of Saturday, 14 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Rio: Chelsea Wataisubua Man City

Rio: Chelsea Wataisubua Man City Rio: Chelsea Wataisubua Man City

NAHODHA wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amesema kuwa Chelsea watawasumbua Man City kwenye ubingwa msimu huu.


Chelsea walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Super Cup juzi baada ya kuwachapa Villareal kwa penalti 5-6, baada ya sare ya bao 1-1.Rio amesema kitendo cha Chelsea kutwaa ubingwa huu wa kinawapa hali ya kujiamini kuwa wanaweza kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Msimu uliopita Chelsea walitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafunga Man City kwenye fainali huku City wakifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Ferdinand amesema mafanikio ambayo Tuchel ameyapeleka Chelsea hakuna ambaye alikuwa anayatarajia.“Jambo ambalo linaonekana sasa ndiyo tofauti ya Man City na Chelsea, hakuna aliyekuwa anatarajia kuwa watakuwa wapinzani msimu uliopita lakini sasa picha inaonekana.

“Lakini naona kuwa Chelsea wanaweza kuwasumbua zaidi msimu ujao kwa kuwa wana makombe mawili sasa na wanachotaka ni kuona wanachukua makombe mengine.

“Naona kuwa Chelsea watakuwa wapinzani wakubwa wa City msimu ujao.“Wameshapata morali ya ushindi, unawaona sasa kila wakitengeneza nafasi inakuwa ya ushindi zaidi kwao kwa kuwa ni jambo la kawaida kwao kushinda,” alisema beki huyo wa zamani.Wakati Rio akisema hivyo, Joe Cole amesema kuwa kama Chelsea watafanikiwa pia kumchukua Romelu Lukaku basi itakuwa faida kubwa kwao kwenye ubingwa msimu ujao

Share this:TweetWhatsApp Related