Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558349

Soccer News of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rivers United yagoma mechi yao na Yanga kurushwa Mbashara

Vikosi vya Rivers na Yanga Vikosi vya Rivers na Yanga

Timu ya Rivers United imegomea vyombo vya Habari Kurusha matangazo ya moja kwa moja(Mbashara).

Kwa maana hiyo mchezo huo utarushwa pasipo kuruhusiwa kwa vyombo vya Habari licha ya jitihada na juhudii kubwa zilizofanyika kuhakikisha wanakubaliana ili kuruhusu matangazo hayo.

Katika taarifa yake, Kituo cha Habari cha Azam Media iliyokuwa imeshafanya maandalizi kuhakikisha mchezo huo unarushwa Mbashara imesema ;

"Tunasikitika kuwaarifu kwamba, hatutaweza kuwaletea matangazo ya moja kwa moja ya mchezo wa CAF Champions League kati ya Rivers United & Yanga

Uongozi wa Azam Media Limited; umejitahidi kwa kila namna kuweza kununua haki za Matangazo hayo toka kwa Rivers United, lakini Imeshindikana kwa sababu Rivers United hawataonesha mchezo huo Mubashara.

Pia Azam Media Limited iliomba ruhusa ya kuutangaza kwa sauti na kupeleka matangazo hayo moja kwa moja kupitia Radio (UFM & TV) lakini pia imeshindikana.

Kupitia kwa wawakilishi wetu walioko Nigeria wakiongozwa na Pascal Kabombe, Azam Media Ltd, itawaletea taarifa mubashara za mechi hiyo kupitia chaneli ya Azam Sports 1 wakati wa matangazo ya Simba Day".

Kwa mujibu wa kanuni za CAF mwenye haki ya matangazo kwa raundi za awali ni timu mwenyeji ila kwa sasa Uongozi wa klabu ya Yanga unapambana walau watanzania wapate matangazo ya mechi hata kwa njia za mitandano ya kijamii.