Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585646

Soccer News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rodgers hana mashaka na Tielemans

Youri Tielemans na Kocha wake Brendan Rodgers Youri Tielemans na Kocha wake Brendan Rodgers

Wakati Youri Tielemans akihusishwa na baadhi ya vilabu kwenye dirisha hili la usajili, kocha wake, Brendan Rodgers wala hashtuki.

Tielemans amebakiza miezi 18 kwenye mkataba wake na Leicester City. Ni kawaida, kwa wachezaji wa kariba ya Tielemans kuvutia vilabu vikubwa barani Ulaya. Swali ni, Youri mwenywe anaonaje hali hii?

Kuelekea mchezo wa muendelezo wa EPL dhidi ya Burnley, Rodgers ameweka wazi kile anachokiona yeye. Kimsingi, hana mashaka yeyote na uwepo wa Tielemans. Licha ya kubakiza muda mfupi kwenye mkataba wake, Brendan anasisitiza ataendelea kufanya nae kazi kama kawaida.