Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572392

Tennis News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Roger Federer kukosekana Australian Open

Roger Federer Roger Federer

Kwa wadau wa mchezo wa tenesi, bila shaka uwezo na burudani ya Roger Federer ni kitu cha kipekee uwanjani.

Federer yupo nje ya uwanja kutokana na majeruhi ya mguu ambavyo yamekuwa changamoto kwa sehemu kubwa kwa mwaka 2020/21.

Kutokana na hali yake, Roger Federer ameweka wazi kuwa anauwezekano mkubwa wa kutocheza mashindano ya Wimbledon pamoja na Australian Open 2022. Hii ni kutokana na muda wa mashindano haya, yeye atakuwa bado anapambana kurejea kwenye hali yake.

Kwa mujibu wa Federer, uwezekano wa yeye kurejea uwanjani ni majira ya joto mwaka 2022.