Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558781

Soccer News of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ronald Koeman hayuko salama Barca

Kocha wa Barcelona, Ronald Koeman Kocha wa Barcelona, Ronald Koeman

Kocha Mkuu wa kikosi cha Barcelona, Mdachi Ronald Koeman huenda akawa katika wakati mgumu ndani ya kikosi hicho baada ya mfululizo wa matokeo mabaya ambayo wanayapata Barca hivi sasa.

Barcelona wametoka kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita dhidi ya Bayern Munich na jana usiku katika mchezo dhidi ya Granada wamepata sare ya goli 1-1 katika mchezo uliopigwa ndani ya uwanja wa Camp Nou.

Koeman alishindwa kubeba kikombe chochote msimu uliopita akiwa na Wacatalunya hao lakini hakuoneshwa mlango wa kutokea.

Rais wa Barcelona Joan Laporta alishawahi kukiri kuwa matamanio yake makubwa ni kumuona Gwiji wa klabu hiyo Xavi Hernandez, akichukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho.

Kuna kila dalili ndani ya muda mfupi ujao Koeman kama hatakua na muendelezo wa matokeo mazuri akatimuliwa kazi ndani ya kikosi hicho.