Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 559030

Soccer News of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ronaldo: Premier Ligi Ngumu

Bruno Fernandes na Cristiano Ronaldo. Bruno Fernandes na Cristiano Ronaldo.

STAA wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amekiri kuwa walikuwa na kazi kubwa kupambana na West Ham United mpaka kupata ushindi, huku akikiri wazi kwamba Premier ni ligi ngumu zaidi.

Man United ilipata ushindi dhidi ya West Ham wa mabao 2-1 ugenini katika mchezo wa Premier League, juzi Jumapili.

Katika mchezo huo, Man United ilipambana kibabe na kupata matokeo huku kipa wa timu hiyo, David de Gea akiokoa penalti na Ronaldo alifunga bao moja.

Ronaldo anacheza Premier msimu huu, baada ya kuondoka ndani ya ligi hii miaka 12 iliyopita.

Staa huyo alisema: “Kila mechi ya Premier League ni lazima upambane kupata pointi tatu, hii inaonesha ligi ni ngumu. Tumeshinda vikwazo vyote leo (juzi) na tukatafuta njia ya kushinda na tukafanikiwa.

“West Ham mara zote huwa ni wagumu, kama unapata nafasi kufika eneo la boksi inabidi upambane kumaliza vizuri kutokana na uimara wao.

“Ila tunatakiwa kuweka akilini malengo yetu kwa kuona tunafanya vizuri kwa kila mchezo. Pamoja tupambane tuwe imara na kuelekeza nguvu zetu kwenye kupambana.”

Man United itacheza tena na West Ham United kesho Jumatano kwenye Kombe la Carabao huku Jumamosi ikitarajiwa kuvaana na Aston Villa kwenye Premier League.