Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 28Article 540280

xxxxxxxxxxx of Friday, 28 May 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rumble in Dar kulisimamisha jiji Ijumaa hii

Ijumaa hii moto utawaka na jiji litasimama kwa muda pale ambapo Watanzania wanne wakienda kuvunja rekodi kwenye pambano la Rumble in Dar 2 la Mei 28. Pambano hilo la kimataifa litapigwa kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki.

Hassan Mwakinyo bondia namba moja nchini mbali na kuwania ubingwa wa Afrika (ABU), endapo atamchapa Anthony Mayala ataweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kumchapa Muangola huyo.

Rekodi nyingine ambazo zinatarajiwa kuvunjwa kwenye pambano hilo kati ya mabaondia wa Burgaria, Joana Nwamerue na Pencho Tsvetkov.

Mabondia hao sanjari na Ardi Ndembo wa Congo Brazzaville pia hawajawahi kupigwa, endapo watapoteza mapambano yao, rekodi zao zitavunjwa kwa mara ya kwanza na Watanzania.

Ndembo atazichapa na Hamisi Palasungulu, Joana atacheza dhidi ya Halima Bandola na Tsvetkov atacheza na Daniel Matefu kuwasindikiza Mwakinyo na Anthony Mayala kutoka Angola.

Mbali na rekodi hizo kuvunjwa, pia pambano la Jongo Jongo dhidi ya Mnigeria, Olanrewaju Durodora litampa rekodi mpya Jongo bondia namba moja ati ya 12 nchini na wa 211 kati ya 977 duniani kwenye uzani wa cruiser.

Mapambano hayo yalipangwa kufanyika Machi 26 na baadaye kuahirishwa kutokana na msiba wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli.

Hakikisha umelipia kifurushi cha Bomba Tsh 19,900 tu kwenye king'amuzi cha @dstvtanzania ili uweze kutazama pambano LIVE hapa @plustvtz kupitia DStv Channel namba 294 kuanzia saa 2 kamili usiku.

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema.

#vyanyumbanihuanziadstv

Join our Newsletter