Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585922

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ruvu Shooting Yatoa Sare na Mtibwa Sugar Ligi Kuu Bara

Ruvu yabanwa mbavu Mabatini Ruvu yabanwa mbavu Mabatini

Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Ruvu walitangulia kwa bao la Abalkassim Suleiman Ali dakika ya 78, kabla ya Ibrahim Ame Mohamed kuisawazishia Mtibwa dakika ya 82.

Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 11 baada ya mechi 12, Mtibwa ikiwa nafasi ya 11 kutokana na kuizidi Ruvu wastani wa mabao, ambayo inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema kuwa uwanja umechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kufanya vizuri.

Ikumbukwe mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.