Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 585988

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ruvu Shooting Yaweka Wazi Usajili Wao

Ruvu Shooting Yaweka Wazi Usajili Wao Ruvu Shooting Yaweka Wazi Usajili Wao

IKIWA imebaki siku moja kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, Ruvu Shooting FC kupitia kwa ofisa habari wake, Masau Bwire, imeweka wazi mchakato wake wa usajili.

Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa rasmi Desemba 16, 2021 kwa kushirikisha timu za Ligi Kuu Bara, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake na kutarajiwa kufungwa leo Januari 15, 2022.

Bwire alisema kuwa: “Nilienda kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kutafuta vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza mpira, nilifanikiwa kuona wachezaji watatu na kwa sasa uongozi upo kwenye mazungumzo ya mwisho na wachezaji hao ili kuweza kukamilisha usajili kwa haraka kabla ya dirisha la usajili kufungwa.”

Ruvu Shooting imekuwa na mwenendo wa kusuasua hivi karibuni baada ya kupoteza mechi saba kati ya 11 walizocheza na wakivuna pointi kumi tu kwa kushinda mechi tatu na kuchomoka na sare moja.