Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 03Article 540823

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Ruvu Shooting na Simba leo, yanenwa mazito

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara inatazamiwa kuendelea saa 10:00 jioni ya leo 3 Juni 2021kwa mchezo mmoja, maafande wa Ruvu Shooting watakipiga na bingwa mtetezi, Simba kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Submitted by George David on Alhamisi , 3rd Jun , 2021 Bernard Morisson wa Simba akiumiliki mpira kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu ambao Ruvu Shooting aliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Massau Bwire amejinasibu kwa kusema kuwa,wanataka kuchukua alama 6 msimu huu na watapiga pale pale panapouma akimaanisha watawafunga tena kama walivyowafunga 1-0 kwenye mzunguko wa kwanza.

Kwa upande mwingine, kocha msaidizi wa     Simba, Selemani Matola amesema wanajua utakuwa mchezo mgumu lakini watapambana kupata alama tatu ili kujiweka kwenyemazingira ya ubingwa zaidi.

Matola pia amethibitisha kuwa, Mlinzi wa kati wa timu hiyo, Joash Onyango atakosekana kutokana na majeraha ya kichwa aliyoyapata kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Kaizer Chiefs uliochezwa jijini Dar kwenye dimba la Mkapa pamoja na Cleotus Chama aliyefiwa na mkwewe Mercy Mukuka

Mchezaji mwingine anayetazamiwa kukosekana ni kiungo Jonas Mkude ambaye amepelekwa kwenye kamati ya Nidhamu ambayo inataraji kuketi tarehe 6 Juni 2021 kujadili tuhuma zinazomkabili na kuzifanyia maamuzi.

Simba wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi nzuri mbele ya Ruvu Shooting wakiwa wameshinda michezo 16 kati ya 19 waliyocheza tokea tarehe 15 septemba 2010 kwenye VPL pekee yake huku wakitoa sare kwenye michezo 2 tu na kufungwa mchezo mmoja wa 26 Oktoba 2020.

Endapo Simba atapata ushindi kwenye mchezo huo basi atafikisha alama 67 na ataendelea kuongoza ligi kwa utofauti wa alama 6 na watani wao Yanga waliopo nafasi ya pili, pia mchezo huo itakuwa wa 27 kwa Simba hivyo atabakisha michezo 3 kufikia mzunguko wa 30 wa sasa.

Kwa upande wa Ruvu Shooting, ipo nafasi ya 10 wakiwa na alama 37 baada ya kucheza michezo 29.

Join our Newsletter