Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559882

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Sahau kuhusu Simba na Yanga, umewasikia KMC ? (+ Video)

Wachezaji wa KMC play videoWachezaji wa KMC

Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC ameweka wazi kuwa kwa sasa timu hiyo haina hesabu za kufikiria mechi za Dabi zitakazowakutanisha dhidi ya Simba,Yanga na Azam FC badala yake nguvu kubwa ni kwenye mechi zote za ligi ili waibuke kuwa mabingwa.

Christina amesema kuwa wana imani kubwa na kikosi ambacho wamekisajili jambo ambalo linawapa matumaini ya kufanya vizuri.

Na iwapo wametokea kukosa ubingwa basi nafasi tatu za juu katika msimamo wa Ligi nao wawemo.