Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 26Article 539854

Soccer News ya

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Said Makapu duh!

Said Makapu duh! Said Makapu duh!

MCHEZAJI kiraka wa Yanga, Said Juma Makapu amesema mabadiliko ya makocha katika kikosi hicho yamekuwa yakimgusa kwa nyakati tofauti.

“Miongoni mwa makocha ambao wamewahi kunipa nafasi ya kucheza zaidi ni Luc Eymael pengine alikuwa anavutiwa na uchezaji wangu au mahitaji ambayo alikuwa anayataka nilikuwa nafiti vizuri,” alisema Makapu na kuongezea;

“Ambavyo nilikuwa napambana na kushindana kati mazoezi au kwenye mechi pindi yupo Eymael ndio hivyo hivyo nafanya wakati huu au mwingine.

“Bado nina imani nitakuja kupata nafasi ya kucheza zaidi kwani nafanya kila ambacho anahitaji kocha tukiwa mazoezini, pia akinipa nafasi kwenye mechi nifanya ambavyo anahitaji,” alisema

Tangu ameondoka Eymael katika kikosi cha Yanga wamepita makocha wanne, Zlatko Krmpotic, Cedric Kaze, Juma Mwambusi na Nabi Mohamed wote Makapu si chaguo lao la kwanza.

Katika kikosi cha Yanga mabeki wa kati ambao wamekuwa wakicheza mara kwa mara ni Bakari Mwamnyeto, Lamine Moro, Dickson Job na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Katika hatua nyingine, Eymael alisema miongoni mwa wachezaji walio na nidhamu katika uchezaji wao pamoja na maisha ya kawaida ni Makapu ndio maana alikuwa akimpa nafasi ya kucheza.

“Makapu hata katika mazoezi ni moja ya wachezaji ambao wanapenda kujituma kama ilivyo kwenye mechi, anashawishi kwa kocha kumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara,” alisema Eymael.

Join our Newsletter