Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558688

Soccer News of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Sakata la kesi ya Morisson CAS lina hoja ndani yake

Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo Duniani CAS wameahirisha kutoa uamuzi wa kesi ya Klabu ya Yanga na Mchezaji Bernard Morrison kutoka leo Septemba 21 hadi Oktoba 26 mwaka huu.

Mmoja ya Mawakili anayewakilisha klabu ya Yanga katika kesi hiyo, Alex Mgongolwa amesema amepokea taarifa ya CAS leo ikieleza sasa hukumu hiyo imesogezwa mbele mpaka Oktoba 26.

"Siku zote ukiona kama hukumu inasogezwa mbele basi mleta shauri ana hoja ndio maana unaona hivyo, kwahiyo tunasubiri maamuzi hayo" amesema Mgongolwa

"Unajua kwa kuwa hii taarifa wao wameileta wenyewe, kwa kuwa wao ndio wana maamuzi juu ya suala hili, sisi tumelipokea na tunawaachia wao wenye maamuzi" amesisitiza

Hii ni mara ya tatu shauri la Morisson na Yanga linaaihirishwa kutolewa maamuzi na Mahakama hiyo ya usuluhishi wa michezo.

Yanga walipeleka shauri lao katika Mahakama hiyo, mwaka 2020 baada ya Shrikisho la Ska nchini TFF, kumpa haki mchezaji huyo ambae aliamua kujiunga na Simba SC.