Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552673

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Salamu za pole msiba wa Mwalimu Kashasha zamiminika

Aliekuwa Mchambuzi wa Masuala ya Soka, Mwalimu Kashasha Aliekuwa Mchambuzi wa Masuala ya Soka, Mwalimu Kashasha

Ikiwa ni siku moja tu tangu kutokea kifo cha Mwanahabari na Mchambuzi mkongwe wa masuala ya Soka nchini Mwalimu Alex Kashasha, wadau mbali mbali wameoneshwa kuguswa na kumlilia mkongwe huyo.

Wadau wengi wamekua wakiongelea uwezo wake na mtindo wake wa utangazaji na uchambuzi na hasa maneno yake, kitu kinachoonesha alikua kipenzi cha wapenda soka hapa nchini.

"mwalimu kashasha ama mzee wa locomotive faint alikua mbunifu na kila siku usingependa kuacha kumsikiliza lakini pia pongezi nyingi kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kukubali kuwa na mtu kama Mwalimu Kashasha". amesema mmoja wa wadau wa michezo.

Marehemu Kashasha muda mwingi alikua akifanya shughuli zake za utangazaji na watangazaji wawili, Jesse John na Enock Bwigane.

"Mwalimu kashasha namfahamu muda mrefu tangu enzi ananisimamia kama kocha wakati nasoma ualimu Butimba, mimi nilikua golikipa wa timu ya Chuo, Kashasha amecheza na anaujua vyema mpira na ameusomea kwa kweli nitamkumbulka na tulikua na Chemistry nzuri sana " amesema Jesse John.

"Ni mimi ndio nilimleta mara baada ya kuachana na Masuala ya Ualimu nikamuomba bwana unapaswa kuwa pembeni yetu hapa uwe unatusaidia na kweli akakubali,niweze kusema alikua ni mtu wa kujituma na kwa umri wake ingekua mwingine angefikiria kupumzika zaidi". ameongeza Jesse John.

Mwalimu Kashasha alijiunga TBC, mwaka 2014 kwa shughuli za utangazaji, na amefanya kazi hizo mpaka mauti yalipomkuta Agosti 19 Jijini Dar es Salaam.