Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 26Article 574114

Soccer News of Friday, 26 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Samatta Afanya Yake Ujerumani

Samatta Samatta

Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunga bao moja katika sare ya 2-2 waliyoipata Royal Antwerp FC ugenini dhidi ya Frankfurt ya Ujerumani, katika mchezo wa kundi D ligi ya Uropa usiku wa kuamkia leo Novemba 26.

Samatta alipachika bao dakika ya 88 kabla ya Frankfurt kusawazisha dakika za nyongeza za mchezo huo. Bao jingine la Royal Antwerp FC lilifungwa na kiungo Radja Naingolan

Matokeo hayo yanaifanya Royal Antwerp FC kufungashiwa virago kwenye michuano hiyo baada ya kusaliwa na alama mbili huku mchezo mmoja ukiwa umesalia na kuwaacha Olympiacos ya Ugiriki na Frankfurt wakifuzu kwenda hatua ya mtoano

Timu nyingine iliyofungashiwa virago katika kundi D ni Fernabache ya Uturuki.