Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 09Article 541744

Michezo Mingine of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Sasa rasmi masomo ya michezo yarejeshwa vyuo Butimba, Mtwara

Sasa rasmi masomo ya michezo yarejeshwa vyuo Butimba, Mtwara Sasa rasmi masomo ya michezo yarejeshwa vyuo Butimba, Mtwara

Katika kuendelea kuboresha michezo na sanaa nchini, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu kurejesha mafunzo ya michezo katika vyuo vya Butimba na Mtwara.

Amesema wahitimu kutoka vyuo hivyo wataajiriwa kufundisha michezo na sanaa katika shule mbalimbali kwani serikali imejidhatiti kuboresha sekta hizo.

Aidha, ameagiza somo la michezo kwa vitendo kutiliwa mkazo mashuleni na ameiagiza wizara hiyo kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza michezo shuleni.

Amesema kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya, ni muhimu wananchi wakajikita kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vingi kutoka na mfumo wa maisha.

Join our Newsletter