Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 21Article 552823

Boxing News of Saturday, 21 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Selemani Kdunda amchapa Kamata kwa K.O

Bondia kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania, Selemani Kidunda Bondia kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania, Selemani Kidunda

Bondia kutoka Jeshi la wananchi Tanzania, Selemani Kidunda amefanikiwa kutetea mkanda wake wa PST baada ya kumpiga mpinzani wake Paul Kamata.

Kidunda alishinda kwa KO raundi ya Saba ambapo zilikua zimebaki sekunde 46 kwa raundi hiyo kukamilika.

Mabondia hao waliokuwa wakipigana katika uzito wa Super Middle Weight katika pambano la raundi kumi.

"Alitumia target vizuri na ameshinda,kama na mimi ningetumia target vizuri bila shaka habari ingekua nyingine" amsesema kamata mara baada ya pambano

Katika pambano hilo Selemani Kidunda alitawala sehemu kubwa ya mchezo huo kuanzia raundi ya kwanza mpaka raundi ya saba aliyopata ushindi.