Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585919

African Cup of Nations of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Senegal Yatoa Sare Tasa na Guinea Afcon 2021

Mchezo wa Senegal vs Guinea umeisha kwa sare ya bila kufungana Mchezo wa Senegal vs Guinea umeisha kwa sare ya bila kufungana

Timu ya taifa ya Senegal imebanwa mbavu ya sare tasa na Guinea katika mchezo wa pili wa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2021 hatua ya makundi Kundi B kwenye mtanange uliopigwa Leo Ijumaa Januari 14.

Matokeo ya Senegal ambao walimaliza nafasi ya pili kwenye mashindano ya Afcon yaliyopita huku Guinea wakiishia nafasi ya 16 bora, yamezifanya timu hizo kuwa karibu kufuzu hatua ya 16 bora.

Matokeo hayo yanaifanya Senegal na Guinea kufikisha alama nne baada ya mechi mbili ambapo mchezo wa mwisho utachezwa baina ya Zimbabwe na Guinea na Senegal na Malawi.

Kocha wa Senegal Cisse amepata sare hiyo huku sababu zake zikieleweka ambapo anaendelea kuwakosa wachezaji muhimu kama mlinda mlango Edouard Mendy nahodha na beki wa kati Kalidou Koilibaly beki Fode Ballo-Toure na kiungo mkabaji Idrissa Gana Gueye wote wakibainika kuwa na virusi vya Covid-19.