Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 560020

Habari za michezo of Monday, 27 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Senzo: Makombe Yote ni Yetu Msimu Huu

Senzo: Makombe Yote ni Yetu Msimu Huu Senzo: Makombe Yote ni Yetu Msimu Huu

KAIMU Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema kuwa kushinda kwao Ngao ya Jamii ni mwanzo mzuri wa kwenda kutwaa makombe yote ya msimu huu.

Senzo alifunguka kuwa hakuna jambo nzuri kwa timu yoyote ile duniani kama kuanza msimu kwa ushindi au ubingwa na jambo nzuri kwao wameanza kwa kuifunga Simba ambao ni watani wao.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Senzo alisema kuwafunga Simba na kuchukua ubingwa ni kitu kikubwa kwao tofauti na watu wanavyofikiria kwa sababu hiyo itawaongezea morali na ari kuelekea kuanza msimu mpya wa ligi.

“Nafikiri hii sasa ni ishara ya kuwa makombe yote ya msimu huu ni ya kwetu, kumfunga Simba na kuchukua kombe ni jambo ambalo linatengeneza kitu cha utofauti kwenye timu.

“Watu wanajua kuwa hatuna mafanikio kwa misimu minne sasa, hivyo huu unakwenda kuwa msimu wa mataji kwa Yanga,” alisema Senzo.

Yanga waliwafunga Simba bao 1-0 na kutwaa Ngao ya Jamii kwenye mchezo ambao ulichezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa.