Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 08Article 584137

Soccer News of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Shiboub, Moukoro Wakabidhiwa kwa Pablo

Shiboub na Moukoro Shiboub na Moukoro

OFISA Habari wa Simba, Ahmed Ally, amefunguka na kuelezea kwamba, suala la wachezaji wote wanaofanya majaribio kikosini hapo, uamuzi wa mwisho wa kusajiliwa kwao upo chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Simba ina wachezaji watatu ambao wanafanya majaribio kwa ajili ya kusajiliwa ambao ni Sharaf Shiboub, Moukoro Tenena na Etop Udoh.

Ahmed alisema: “Wachezaji waliokuja kufanya majaribio wataangaliwa na mwalimu na mwalimu atatoa takwimu zao, kama watakuwa wamekidhi vigezo basi tutawasajili.

“Tunaiheshimu sana michuano ya Mapinduzi na tunatamani kulichukua kombe ndiyo maana hakuna mchezaji aliyepewa likizo.

“Tumekuja na kikosi chote hata Lwanga (Taddeo) na Nyoni (Erasto) ambao walikuwa majeruhi na wanatarajiwa kuanza kucheza mwishoni mwa mwezi huu.”

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola alisema: “Wapo wachezaji wapya ambao wanacheza kwa sasa wapo kwenye majaribio lakini bado wapo kwenye matazamio ili tuweze kujua kile walichonacho na imekuwa hivyo kuwafanyia wachezaji ambao tunahitaji kufanya nao kazi.

“Ikiwa utamuona mchezaji kwenye mchezo mmoja hapo huwezi kutoa hatma yao kwa kuwa bado kuna mechi nyingine ambazo wanapaswa kucheza pamoja na kuangalia kile ambacho wanakifanya uwanjani,” alisema Matola.