Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 585931

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Si unampamba Sakho ? Msubiri katika mechi hizi ..

Pape Ousmane Sakho Pape Ousmane Sakho

Inakuwa rahisi kwa mpira wetu mchezaji kuanza kuimbwa jina lake mapema sana, inakuwa rahisi pia kuanza kumponda inapogundulika kuwa anayoyafanya ni nguvu za soda.

Kuliko kuingia katika mkumbo huo wa kishabiki busara ni kumpa muda wa kutosha Pape Osman Sakho kabla ya kuanza kuliimba kwa mbwembwe jina lake.

Wapo wanaojaribu kumlinganisha Sakho na Luís Miquissone, winga wa Al Ahly, kiuchezaji misingi yao ya kimpira ipo tofauti. Sakho ni mchezaji kutokea Afrika Magharibi wakati Miquissone ni kutokea Msumbiji. Ipo tofauti kubwa kati ya Senegal na Msumbiji.

Ni afadhali Sakho akatazamwa mchango wake wakati wa zile mechi za Ligi Kuu zinapokuwa zimeshachanganya.

Wakati huo Yanga na Simba wakiwa wanautafuta ubingwa, na zimebaki mechi kama kumi ligi kuu imalizike na bingwa ajulikane. Hapo ndipo uwezo halisi wa Sakho utakapoonekana. Wakati mabeki wakiwa wanampania.

Maana ipo tabia ya mabeki hasa wazawa kupenda kumsubiri mshambuliaji anayekuwa midomoni mwa mashabiki akiimbwa na kujazwa sifa.

Wao hutaka kumwonyesha mchezaji husika na wale wanaoliimba jina lake kwamba ni wa kawaida tu. Hapo mchezaji maarufu anakuwa anapimwa kama kweli kiwango chake ni kikubwa kama kinavyosemwa au ameongezewa chumvi.

Miquissone alicheza mechi ngumu dhidi ya Al Ahly na akafunga goli la viwango vya kimataifa. Alizicheza mechi nyingi zenye mabeki wanaojua kuzikamia Simba na Yanga. Alikutana na mitihani na akaifaulu vizuri.

Kumlinganisha na Sakho ambaye inasemekana ndiyo kwanza amepona majeraha aliyokuja nayo Simba kwa kweli ni mapema mno.

Mapinduzi Cup na Ligi Kuu ya Bara ambayo ni ndefu na yenye ugumu wake ni michuano miwili tofauti kabisa. Japokua kuibuka mchezaji bora wa Mashindano hayo sio jambo la kubeza hata kidogo

Nazitunza sifa zangu mpaka zikipita mechi kadhaa ndiyo nitaona kama Sakho ni mrithi halisi wa Luis Miquissone au kwa kuwa amekutana na mchekea, Mapinduzi Cup.