Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 22Article 552916

Soccer News of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Sifikirii Kuondoka Yanga kwa sasa" - Mukoko

Kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe Kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe

Kiungo wa Wanajangwani Mukoko Tonombe "teacher" ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa zinazosambaa mitandaoni kudai kuwa amegomea mazoezi ya timu hiyo na anashinikiza kuondoka katika klabu hiyo kwa kuwa amepata ofa na moja ya klabu kutoka nchini Morocco.

Nyota huyo amewatoa hofu wanayanga na kuwataka watulie kwa kuwa Yanga yeye ni nyumbani na hajapata ofa yoyote itakayomfanya aondoke yanga.

Akizungumza na Mwanaspoti katika kambi ya timu hiyo iliyopo Marrakech, Mukoko amesema kutoonekana kwake katika mazoezi ya kikosi hicho tangu afike ni kwa sababu za kitabibu na sivyo kama inavyozungumzwa kuwa anashinikiza kuondoka.

Mukoko ambaye amebakiza Mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu ya Yanga mpaka kufikia sasa amesema "focus" yake ni kuisaidia yanga kupata kile wanachohitaji.

“Mi sina ofa ambayo imenifanya nigome, nyinyi waandishi mpo hapa mmeona nafanya mazoezi hapa nikiwa na daktari huwa nasumbuliwa na kichwa na hata kule Tanzania niliwahi kuugua hivi kama mnakumbuka,” amesema staa huyo

“Kama kuna ofa huwa tunazungumza na Yanga tunapima na kujadiliana, lakini mimi ni mchezaji wa Yanga haya maneno ya mitandaoni watu wa Yanga wanatakiwa kuachana nayo, mimi nipo hapa sana.”

Katika mazoezi ya juzi jioni Mukoko ameonekana kwa mara ya pili tangu Yanga ilipowasili Morocco, na ameonekana akikimbia nje ya uwanja huku akisimamiwa na daktari Sheicky Mngazija kisha baadaye alinyoosha viungo na kutakiwa kutulia, ratiba ambayo aliendelea nayo siku iliyofata.