Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553807

Soccer News of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Sijatoa siri za Simba nimeanika uonevu wa Mabosi wao" - Manara

Msemaji wa Yanga, Haji Manara Msemaji wa Yanga, Haji Manara

Msemaji wa Klabu Kongwe ya Soka nchini Yanga, Haji Manara ametolea ufafanuzi kauli za mashabiki wa Soka nchini wanaodai ametoa siri za Klabu iliyomuajiri na kumpa dhamana kama Msemaji wao lakni leo anashindwa kuwa muadilifu dhidi yao hivyo wanamuita msaliti.

Manara ametolea ufafanuzi huo alipofanya mahojiano leo Agosti 26 na kituo cha Redio cha Wasafi Fm ambapo amesema sio kweli kama ni msaliti wala hajatoa siri yoyote ya simba kwani zipo nyingi tu anazozijua na hajafungua kinywa kuzungumza.

"Mimi sijatoa siri za Simba, nimezungumza niliyokua nafanyiwa na mabosi wao "Mo" na Babra, wakae wajue kutofautisha mi nilikua na bado mtiifu kwa simba guys lakini muda si mrefu watakuja kujua".

"Mabosi wao wamenifanyia vitu vingi sana vya hovyo ili kuniondoa katika klabu, kwa hiyo mpaka nimeondoka wajue nimestahimili mengi na yote ni kwa sababu ya Simba" amesema Manara

Manara aliachana na Simba mwezi uliopita na siku Mbili zilizopita ametambulishwa kama msemaji mpya ndani ya klabu ya Yanga.