Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585634

Soccer News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Simba Bingwa Mapinduzi Cup 2022, Refa aacha gumzo

Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2022, Simba Sports Club Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2022, Simba Sports Club

Ndio wameandika Historia. Simba SC wamebeba Kombe la Mapinduzi baada ya kuitandika Azam FC kwa goli 1-0 katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Hapo awali Simba ilipata kuingia fainali kadhaa za Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC lakini walijikuta wakipoteza lakini hii leo Kocha Pablo Franco ameandika historia mpya.

Goli pekee la ushindi katika mchezo huo limefungwa kwa mkwaju wa Penati na mshambuliaji Meddie Kagere kunako dakika ya 55 ya mchezo baada ya makosa ya mlindo mlango wa Azam, Mathias Kigonya kumchezea madhambi Sakho.

Mchezo huo ulitawaliwa na ufundi na kasi ya hali ya juu mpaka zinakamilika dakika 90 ni Simba ndio waliofanikiwa kujinyakulia taji lao la kwanza msimu huu.

Katika mchezo wa Fainali kulikuwa na maauzi kadhaa yaliyofanywa na mwamuzi ambayo walio wengi wlikua na mashaka nayo.