Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 27Article 554026

Soccer News of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba Day September 19 kwa Mkapa

Tarehe ya Tamasha la Simba Day Tarehe ya Tamasha la Simba Day

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wametangaza tarehe rasmi watakayofanya Tamasha kubwa la kimichezo maarufu kama "Simba Day".

Katika taarifa yao iliyotolewa kwenye mitandao yao ya kijamii, Simba wameandika;

"Tarehe ya tukio kubwa zaidi la michezo nchini ni Septemba 19, 2021 siku ya jumapili kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam".

Tukio la Simba Day, kila mwaka hufanyika Agosti 8, Lakini kutokana na kubana kwa ratiba imebidi kuchelewa katika maadhimisho yake, na katika Tamasha hilo ndipo ambapo wachezaji wapya hutambulishwa.