Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 27Article 553999

Soccer News of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba Jijini Dar wikendi hii

Kikosi cha Simba kikijifua Kikosi cha Simba kikijifua

Mabingwa Ligi kuu Tanzania bara, Simba SC, wanatarajiwa kufunga kambi yao wiki hii na kurejea katika ardhi ya Dare es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa Habari, wakati wa kuzindua "App" ya Simba, Kaimu Afisa habari wa Klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema timu hiyo itawasili nchini wikiendi hii na wachezaji watapewa mapumziko ya siku 1-2 kisha watajiunga na kambi awamu ya pili kujiandaa na Msimu mpya wa Ligi na ule wa Klabu bingwa barani Afrika.

Kamwaga hakusema wazi kuwa Kambi hiyo itakuwa wapi na itakuwa kwa muda gani lakini alisisitiza tu wanachama wapakue "App" na taarifa zote watazikuta humo.

Simba mpaka sasa ipo nchini Morocco ikijifua kwa maandalizi ya msimu ujao na kitendo cha kurudi ni wakati wa kuwapa Mashabiki nafasi ya kuwaona nyota mpya waliosajiliwa na Klabu hiyo.