Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585607

Soccer News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Simba: Majaribio ni Muhimu

Simba: Majaribio ni Muhimu Simba: Majaribio ni Muhimu

KLABU ya SImba imesema majaribio kwa wachezaji wageni kabla ya kuwasajili ni muhimu kwani Simba ni Klabu kubwa haiwezi kusajili wachezaji pasipo kujiridhisha ubora wa viwango vyao.

“Niwakumbushe Simba SC tumewahi kuwafanyia majaribio wachezaji wengi sana hapa nchini, tumefanya kwa Lamine Moro ambaye kwetu hakuonekana anafaa, lakini kwa wenzetu walitumia mpango wetu na walimsajili na kisha walimpa hadi unahodha,”

“Kipindi hiki cha Dirisha Dogo tumeona tuitumie michuano ya Mapinduzi kuwafanyia majaribio hawa wachezaji na tumefanikiwa, huu ni mfumo wetu sisi kama Simba SC kama wengine hawautumii basi, lakini sisi tunajua tunachokifanya kupitia kwa kocha wetu Franco Pablo Martin,” amesema msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally.