Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 27Article 540106

Habari za michezo of Thursday, 27 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Simba: Moto wetu ni ule ule

Simba: Moto wetu ni ule ule Simba: Moto wetu ni ule ule

Bocco ambaye alifunga mabao mawili katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs alisema wataendelea kujituma kwenye kila mchezo kwa sababu wanahitaji kutimiza malengo ya kutetea mataji yote mawili wanayoyashikilia.

Mshambuliaji huyo alisema wanafahamu mechi zilizosalia ni ngumu kutokana na kila timu kusaka matokeo chanya na hatimaye kufikia malengo.

"Bado hajutamaliza msimu, tutaendelea na mapambano katika mechi zetu zote zilizosalia, tunahitaji kutetea ubingwa wa Ligi Kuu na sisi pia ndio tunashikilia Kombe la FA, nafasi iko wazi, hatutakiwi kupoteza mchezo," alisema mshambuliaji huyo.

Aliongeza kila mchezaji wa Simba anatamani kuona tunamaliza msimu kwa mafanikio na kuwafuta machozi mashabiki wetu baada ya kuondolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya mechi ya jana usiku ya Kombe la FA dhidi ya Dodoma Jiji FC, kikosi cha Simba kitajiandaa na safari ya kuelekea Lindi kuwafuata Namungo FC kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Majaliwa.

Join our Newsletter