Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 31Article 554623

Soccer News of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba Queens kuendeleza Ubabe CECAFA

Kikosi cha Simba Queens Kikosi cha Simba Queens

Wawakilishi pekee kutoka Tanzania katika michuano ya Caf Women's Champions League Cecafa Qualifiers 2021, Kikosi cha Simba Queens Leo Agosti 31 saa 10 jioni kitashuka katika uwanja wa Kasarani kuikabili Lady Doves kutoka Uganda.

Katika Mchezo wa Kwanza, Kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi kiliibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya PVP FC.

Akizungumza kuelekea mchezo huo Kocha mkuu wa Kikosi hicho ameeleza ni kwa kiasi gani wamejipanga kuhakikisha wanafanya vyema katika mchezo huo.

"Tunahitaji kushinda dhidi ya Lady Doves, tukishinda tutakuwa tumekata tiketi ya kuingia nusu fainali na malengo yetu ni kushinda taji hili baadaye twende Misri" amesema Kocha Hababuu.

Simba Queens ipo kundi A sambamba na timu za PVP FC (Burundi), LADY DOVES WFC kutoka Uganda, FAD FC (Djibout).